Waamua vita ya jua na mwezi, Upepo na mawimbi vyakujua,
Uketiye mahali pa siri, Patakatifu palipoinuka,
Wautangaza mwisho mwanzoni, Hakuna usilolijua.
Ufalme wako ni wa zamani zote vizazi vyote.
Vizazi kwako si ukomo, (Vizazi kwako si ukomo),
Miaka kwako sio umri, (Miaka kwako sio umri),
Vizazi kwako si ukomo, (Vizazi kwako si ukomo).
Wadumu milele, (Wadumu milele),
Wadumu milele, (Wadumu milele),
Wadumu milele, (Wadumu milele).
Maji yenye kina kirefu, Kamwe hayapigi kelele,
Ni kweli kuna mabwana wengi, Lakini wewe ni Bwana wa mabwana,
Ni kweli kuna miungu mingi, Lakini wewe ni Mungu wa miungu,
Hufikiwi kwa mnara wa Babeli,Jina lako ni ngome imara.
Ufalme wako ni wa zamani zote vizazi vyote.
Nani wa kulingwanishwa nawe Jehova mwenye nguvu;
Ufalme wako ni wa zamani zote vizazi vyote.
Vizazi kwako si ukomo, (Vizazi kwako si ukomo),
Miaka kwako sio umri, (Miaka kwako sio umri),
Bwana, vizazi kwako si ukomo, (Vizazi kwako si ukomo).
Umejawa nazo siku nyingi, (Wadumu milele),
Mwanzo na mwisho viko ndani yako, (Wadumu milele),
Umeshiba siku na utajiri, (Wadumu milele),
Wadumu milele, (Wadumu milele),
Wadumu milele, (Wadumu milele),
Bwana wadumu milele, (Wadumu milele),
Bwana, wadumu milele, (Wadumu milele).
Yeah, (Yeah)
Yeah, (Yeah)
Yeah, (Yeah)
Say, Yeah, (Yeah)
Yeah, (Yeah)
Yeah, (Yeah)
Yeah, (Yeah)
Ufalme wako ni wa milele yote Bwana.